WANAFUNZI 32,153 KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2018, MKOA WA GEITA WASHIKA NAFASI YA PILI KITAIFA MATOKEO DARASA LA SABA 2017
Wanafunzi 32,153 kati ya 36,979 waliosajiliwa kufanya mtihani wa Darasa la Saba Mwaka 2017 Mkoani Geita wamechaguliwa kuendelea na elimu ya Sekondari mwaka 2018 (Kidato cha kwanza).
Akitangaza matokeo hayo kwa ngazi ya Mkoa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Bw. Selestine Gesimba amesema wanafunzi 32,153 (Wav. =16110 na Was.=16043) wamefaulu Mtihani wa Darasa la Saba na kufanikiwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule mbalimbali za Sekondari sawa na asilimia 98% ya wanafunzi 36,979 waliosajiliwa kufanya mtihani. Watahiniwa ambao hawakufanya Mtihani ni 391 sawa na asilimia 1.05% kwa sababu za utoro, ugonjwa na vifo vya wanafunzi pamoja na sababu nyingine.
Katibu Tawala amesema kuwa ufaulu wa Mkoa umeongezeka kwa asilimia 0.3 kutoka 86.92 mwaka 2016 hadi kufikia asilimia 86.95 kwa Mwaka 2017 huku wastani wa ufaulu ni alama 146.17 hivyo kuufanya Mkoa wa Geita kushika nafasi ya Pili Kitaifa nyuma ya Mkoa wa Dar es salaam ambao ndio kinara kitaifa.
Matokeo haya yanaonyesha kuwa Halmashauri za Mkoa wa Geita zimefanya vizuri kitaifa zikiongozwa na Halmashauri ya Wilaya ya Chato iliyoshika nafasi ya 10, Geita Mji nafasi ya 16, Bukombe nafasi ya 17,Nyang'hwale nafasi ya 22, Mbogwe nafasi ya 26 na Geita Vijijini nafasi ya 29 kitaifa kati ya Halmashauri 184.Kupata Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa na Shule waendazo bonyeza hapa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa