Mkuu wa mkoa wa Geita mhe.Rosemary Senyamule ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Geita kuchangamkia fursa iliyotolewa na Benki ya CRDB ambayo itaweza kuwanufaisha kiuchumi kutokana na faida ilizonazo.
Mhe.Senyamule ameyasema hayo Mei 20, 2022 wakati akizindua bidhaa mpya iitwayo Mzigo Flexi ya Benki ya CRDB akiwa tawi la Geita huku akiwapongeza benki hiyo kwa kuwa wabunifu akiwasihi kwenda mtaani kukutana na wananchi na kuwapa elimu juu ya kuweka akiba
“hongereni sana CRDB mmeonesha kujali wananchi na wateja wenu. Elimu hii iwafikie wananchi na wachimbaji kwani Geita watu ni wachapa kazi na fedha wanazo. Hivyo nitoe wito kwa wananchi, changamkieni fursa ya Mzigo Flexi”. Alimaliza mkuu wa mkoa
Akitoa maelezo juu ya huduma hiyo, ndg.Abel Dai ambaye ni Afisa Mikopo wa Benki ya CRDB Geita alisema, bidhaa hiyo ni ofa itakayodumu kwa muda wa miezi miwili tu kuanzia tarehe 17 Mei hadi Julai 17, 2022 yenye faida ya 9% ya uwekezaji ambayo mteja ataweza kuwekeza kuanzia Milioni 1 na kuendelea na atakuwa ana uhuru wa kuchukua faida kwa mwezi, robo mwaka, nusu mwaka, mwaka na muda wa kikomo tofauti na zamani, hivyo kuwahamisha wateja kuchangamkia fursa hiyo.
Akitoa salamu kwaniaba ya Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi ndg. Anslem Mwenda alisema uzinduzi wa bidhaa hiyo ni mkombozi kwa mtanzania kwani mteja atapa faida bila jasho kisha kumalizia kwa kaulimbiu “Ulipo Tupo”
Mfanyabiashara na mwananchi wa Geita ndg. Atanas Ignas naye akatumia fursa hiyo kutoa ushuhuda wa uwekezaji kwenye Benki ya CRDB kwa wateja na wananchi wa Geita akiwasihi kuitumia fursa kwani wao kama wafanya biashara ina manufaa kwao na kwamba CRDB imewatengenezea mazingira mazuri kuwekeza bila jasho.
Geita ya Dhahabu, Utajiri na Heshima. Kazi Iendeleee
Imeandaliwa na:
Boazi Mazigo
Ag.HGCU
Geita RS
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa