Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Mhandisi Robert Gabriel ameendelea kuwasisitiza wananchi wa Mkoa wa Geita hasa wanaume kujitokeza kwenda kupima afya zao ili kujua kama wana maambikizi ya VVU ili endapo wakugundulika kuwa na maabukizi hayo basi haraka waanze kutumia dawa za kufubaza makali.
Amesema hayo wakati akizindua kampeni ya Kitaifa ya Furaha Yangu yenye kusema “Pima, Jitambue, Ishi" na kuhutubia wananchi waliohudhuria uzinduzi huo katika uwanja wa CCM uliyopo Mamlaka ya Mji Mdgo Katoro tarehe 20.10.2018
Amesema, “miongoni mwa malengo ya kampenii hii ni kupambana na maambuziki mapya ya virusi vya UKIMWI (VVU) katika jamii, kuwafikia, kuwapima, kuwapa elimukinga (tohara ya wanaume) na kuanzisha dawa za ARV mapema wale wote wanaogundulika kuwa na maambukizi”. Katika hili Mhandisi Gabriel amesema,“wanaume wote wanisikie mwenzao nazungumza kuwa, tohara ndiyo mpango mzima, kukwepa tohara siyo dili”. Viongozi wa dini pia wahimihizwa kuwa sehemu ya hamasa kwa wanaume.
Mhandisi Gabriel amesisitiza kuwa kampeni inawalenga watanzania wote watambue hali zao lakini zaidi wanaume kwakuwa takwimu za utafiti wa viashiria vya VVU na UKIMWI nchini wa mwaka 2016/2017 umeonyesha kuwapo na kiwango cha chini cha upimaji VVU kwa wanaume ukilinganisha na wanawake jambo linalosababishwa na wanaume kutumia matokeo ya wenza wao, Mhandisi Gabriel akakemea tabia hiyo.
Kabla ya kumaliza hotuba yake, Mhandisi Gabriel ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ofisi ya Rais –TAMISEMI pamoja na wadau wa maendeleo wakiwemo PEPFAR, Mfuko wa Dunia wa Kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria na Jumuiya ya Umoja wa Mataifa kwa kuwezesha uwepo wa Vitendanishi na dawa za kutosha kwa wote wanaohitaji huduma hizo. Lakini pia ameshukuru mchango wa wadau wengine ambao ni Shirika la Maendeleo la Marekani USAID kupitia Mradi wa Tulonge Afya, Shirika la Kimataifa la Kazi Duniani (ILO), Asasi za Kiaria za Kupambana dhidi ya UKIMWI, wakiwemo Jhpiego, ICAP, INTRA-HEALTH TANZANIA, MDH, TAYOA, Benjamin Mkapa Foundation, AMREF, PSI na University of Maylanda bila kuwasahau viongozi wa dini ya vyama vya siasa, kisha kwenda kutembelea mabanda ya kutolea huduma za afya kiwanjani hapo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Josephat Maganga kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kutoa hotuba yake, alieleza kuwa miongoni mwa changamoto inayoonesha namba kubwa ya waathirika wengi kutoka Wilayani Geita ni kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu kutokana na shughuli za madini ya dhahabu.
Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa shughuli za udhibiti UKIMWI Daktari Japhet Simeo ambaye ni Mganga Mkuu wa Mkoa alisema, “uzinduzi wa kampeni ya Furaha Yangu, Pima, Jitambue, Ishi ulifanyika tarehe 19.06.2018 uliofanywa na Waziri Mkuu Mhe. Kasism Majaliwa ambapo shughuli hiyo mkoani Gieta hufanyika leo, ambapo tarehe kama ya leo tutakuwa tukikumbushana juu jamii ya janga la UKIMWI katika jamii yetu kwa kuzingatia yafuatayo yakiwemo kupima afya na kujijua na kuanza dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI na kuhamasisha wanaume wote katika Mkoa wa Geita wajitokeze kwa wingi kupima na kuacha kutumia majibu ya wenza wao”.
Mganga Mkuu pia amesema kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2012/2013, asilimia arobaini na nne (44.6%) ya wanaume wenye umri wa zaidi ya Miaka Kumi na Nane hawajatahiriwa jambo ambalo huweza kusababisha maambukizi kwa asilimia sitini (60%).
Shughuli hiyo ya uzinduzi imehudhuliwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti wa Chama Tawala CCM Mkoa, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Idara ya Vitengo Sekretarieti ya Mkoa, Washiriki kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Wawakilishi wa Wadau wa Maendeleo, Waratibu wa Huduma za Afya, Wafanyakazi wa Sekta zote, Wanahabari
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa