Na Boazi Mazigo - Geita RS
Ikiwa ni siku ya tatu tangu kuwasili mkoani hapa, Katibu Tawala Mkoa Geita Bw.Mohamed Jumanne Gombati amelakiwa na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kisha kuzungumza nao ikiwa ni mara yake ya kwanza kuonana nao tangu ateuliwe na kuripoti katika kituo chake cha kazi.
Mapokezi hayo ya RAS Gombati yamefanyika Oktoba 2, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita-Magogo ambapo watumishi wa umma wamehimizwa kuwa wabunifu, wachapa kazi, wenye ushirikiano lakini bila kusahau uadilifu.
“niwashukuru kwa mapokezi lakini nisisitize juu ya uwajibikaji, uadilifu na niombe ushirikiano wenu ili kutekeleza majukumu vizuri. Dira yetu ni kuwa sekretarieti ya mfano katika utoaji wa huduma, na hiyo tutaifanikisha ikiwa tutafanya kazi kwa bidii na kuwa wabunifu”. Alisema RAS Gombati.
Aliongeza kuwa, ni muhimu kuzingatia thamani ya miradi, lakini pia amesisitiza juu ya kufanya kazi kwa haraka lakini kwa usahihi na kwamba si vyema kwa watumishi kuchukua mda mrefu kushughulikia mafaili.
Na mwisho, RAS Gombati amewataka watumishi kuhakikisha wanashughulikia hoja kabla ya kusubiri taarifa ya CAG akiamini uwezo huo upo na kuwasihi watumishi kuwashauri viongozi kwa usahihi.
Ikumbukwe kuwa, Bw. Mohamed Gombati alikabidhiwa ofisi rasmi Septemba 30, 2023 na Prof.Godius Kahyarara ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wizara ya Uchukuzi.
Geita ya Samia, Hakuna Kilichosimama.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa