WAZIRI MKUU ATEMBELEA WILAYA YA CHATO AZINDUA OFISI YA TRA
Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya ziara ya siku mbili Wilaya ya Chato Mkoani Geita na kuzindua Ofisi mpya ya mamlaka ya mapato (TRA).
Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Tanzania amezindua jengo jipya la mamlaka ya mapato Wilaya ya Chato lenye thamani ya shilingi bilioni 1.4 kwa lengo la kusogeza huduma za ulipaji kodi na ukataji wa leseni karibu na wananchi wa Wilaya hiyo ambao walikuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo katika Wilaya ya Geita.
Kabla ya uzinduzi huo Mheshimiwa Kassim Majaliwa aliwataka wananchi pamoja na wafanyabiashara kujenga utaratibu wa kulipa kodi bila ya kushurutishwa ili mapato yatakayopatikana yasaidie kupeleka huduma za kijamii katika maeneo mengine yenye mahitaji. Aidha, ameitaka mamlaka ya Mapato kukusanya kodi za majengo katika majengo yote ya mijini yanayostahili kulipiwa kodi hiyo basipo kuwabughudhi wazee walio na umri zaidi ya miaka sitini (60).
Vile vile amewataka wananchi kufuga mifugo michache kulingana na eneo lililopo ili kuacha tabia ya kuingiza mifugo katika hifadhi za taifa kwa kuwa mazingira yanaharibiwa na kusababisha ukame ambao uleta upungufu wa mvua na baadae upungufu wa chakula katika baadhi ya maeneo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa