• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Geita Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Geita

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
      • Mikakati
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Maji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • TEHAMA
      • Mkanguzi Wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Geita
    • Bukombe
    • Chato
    • Mbogwe
    • Nyang'hwale
  • Halmashauri
    • Halamashauri ya Wilaya Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
    • Halmashauri ya Mji Geita
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
      • Hifadhi ya Taifa ya Rubondo
    • Uchimbaji wa Madini
    • Ufugaji
    • Ufugaji wa Nyuki
    • Kilimo
    • Maeneo ya Viwanda
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma Ufugaji
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

WAZIRI NDALICHAKO ATEMBELEA SHULE YA SEKONDARI MAGUFULI ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA LIPA KWA MATOKEO(P4R).

Posted on: January 1st, 2018

WAZIRI NDALICHAKO ATEMBELEA SHULE YA SEKONDARI MAGUFULI  ARIDHISHWA  NA UTEKELEZAJI  WA MIRADI YA LIPA KWA MATOKEO(P4R)

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Pro.Joyce Ndalichako amefanya ziara fupi Wilayani Chato kwa kuitembelea Shule ya Sekondari Magufuli na kukagua utekelezaji wa miradi ya lipa kulingana na matokeo(P4R) shuleni hapo.

Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa mabweni, Bwalo, vyoo na vyumba vya madarasa Profesa Joyce Ndalichako ameupongeza Uongozi wa Mkoa, Halmashauri ya Chato na Shule ya Sekondari Magufuli kwa kusimamia vizuri fedha za utekelezaji wa miradi hiyo kwa ubora na kiwango kinachotakiwa.''Nafurahi kuona fedha za P4R zinatumika kwa matumizi yaliyokusudiwa kama tulivyokagua na kujionea kiwango kilichojengwa ndio haswa kinachotakiwa ambacho darasa lazima liwe na silling bodi, umeme lakini pia liwe na madirisha tofauti na madarasa tuliyokuwa tunajenga zamani hivyo nawapongeza kwa dhati kabisa viongozi mmefanya kazi kubwa thamani ya fedha inaonekana''.

Profesa Ndalichako amesema Serikali ya awamu ya tano inajukumu kubwa la kuhakikisha kunakuwa na mazingira bora katika utoaji wa elimu hivyo miradi ya namna hii inatekelezwa katika Halmashauri nchi nzima. Amesema mwezi desemba 2017 serikali imetoa kwa halmashauri zote shilingi bilioni 15 na milioni 900 za kuendeleza jitihda za kuimarisha miundombinu ya sekta ya elimu ili kuongeza na kuimarisha majengo kwa ajili ya kupokea wanafunzi wa darasa la kwanza ambapo zitajenga jumla ya madarasa 415, mabweni 46, matundu ya vyoo 814 na mabwalo 7.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi amempongeza Waziri wa elimu kwa kutembelea shule hiyo ili kujionea kazi nzuri iliyofanyika  licha ya kuwa na majukumu mengi ya kitaifa. Amewashukuru wananchi wa Mkoa wa Geita kwa jitihada zao za kushiriki katika ujenzi wa nyumba vya madarasa 8000  kwa shule za msingi na Sekondari ambapo tangu mkoa uzindue kampeni ya ujenzi huo zaidi ya vyumba 900 vya shule za msingi na zaidi ya 130 vya Sekondari vipo katika hatua tofauti. Amesisitiza kuendelea kuunga mkono jitihada zao kwa kuhakikisha kunakuwa na uwazi katika michango inayotolewa na wananchi.

Mhandisi Robert Gabriel amemhakikishia Waziri wa Elimu kuwa pamoja na kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi walioandikishwa kujiunda na elimu ya awali, darasa la kwanza na Sekondari hakutakuwa na mwanafunzi atakaye kaa nje ya darasa kwa kuwa jitihada za zinafanyika kwa haraka ili kukabiliana na hali hiyo.

Akiwa katika shule hiyo Mheshimiwa Waziri wa elimu alikagua ujenzi wa vyumba 8 vya madarasa, matundu 20 ya vyoo, mabweni 2 ya kulala wanafunzi na bwalo  miradi yote hii imetekelezwa na Serikali kupitia mpango wa lipa kulingana na matokeo kwa gharama ya shilingi 570,500,000/=.

Matangazo

  • KANUNI MPYA ZA CSR ZA 2023 August 12, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Wapatieni Wananchi Taarifa Sahihi za Miradi ya Maendeleo- Msigwa

    May 26, 2025
  • Wapatieni Wananchi Taarifa Sahihi za Miradi ya Maendeleo- Msigwa

    May 26, 2025
  • Mkoa wa Geita Kinara Utekelezaji wa Miradi ya TASAF

    May 27, 2025
  • Serikali Inathamini Vyama vya Ushirika- RC Shigela

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Sekta ya Elimu Yazidi Kuimarika Geita
Video Zaidi

Muunganiko wa Haraka

  • Halmashauri ya Wilaya Bukombe
  • Halmashauri ya Mji Geita
  • Halmashauri ya Wilaya Geita
  • Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
  • Halmashauri ya Wilaya ya Chato
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
  • E-VIBALI

Tovuti Zinazohusiana

  • IKULU
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • NECTA
  • NACTE
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Maeneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita

    Sanduku la Barua: S.L.P 315

    Simu: 028 2520035

    Mobile: 028 2520035

    barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa