Na Boazi Mazigo, RS Geita.
Katibu Tawala Mkoa Geita Bw.Mohamed Gombati amewataka watumishi wa umma mkoani hapa kuzingatia maadili na kutoa huduma bora na yenye viwango na kwa wakati huku wakiwa watii kwa serikali.
Bw.Gombati aliyaeleza hayo Oktoba 30, 2023 wakati akizungumza na watumishi wa ofisi ya mkuu wa mkoa geita katika kutekeleza utaratibu wake wa kukaa na kusikiliza kero, maoni na ushauri kutoka kwa watumishi.
"Jueni mnao wajibu wa kutoa huduma iliyo bora kwa wananchi, jiridhisheni na maamuzi mnayoyafanya, itiini serikali, lindeni viapo vyenu na epuka kutoa taarifa za serikali ambazo ni za siri", alisema Bw. Gombati.
Aliongeza kuwa, ni muhimu kwa watumishi kutoa huduma bila upendeleo lakini pia kuzingatia tarehe za mwisho wa utekelezaji maagizo na maelekezo ya viongozi.
Mwisho, Bw.Gombati alisema, serikali inaendelea kuboresha masuala mbalimbali ya kiutumishi; hivyobasi ni vyema watumishi warudishe shukran kwa Mhe.Rais.Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa kupata matokeo chanya ya utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Nao watumishi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa kwa nyakati tofauti wameahidi kutekeleza maelekezo na ushauri uliotolewa na kushauri masuala mbalimbali ya kiutumishi kuendelea kushughulikiwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Sanduku la Barua: S.L.P 315
Simu: 028 2520035
Mobile: 028 2520035
barua pepe: ras.geita@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2017Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita. Haki zote zimehifadhiwa